Tafuta
Kuhusu Sisi
Karibu Mwafika Asili - Blog ya Utalii wa Ndani
Habari Maarufu
Haki Miliki
© 2013 mwafikasil.blogsport.com
Mawasiliano
mwafrikasili@gmail.com
Powered by Blogger.
Saturday, October 22, 2016
12:58 PM
| Imetumwa
MWAFRIKASILI
|
ZIWA NGOZI
Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini na 33.553°Mashariki, ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya lile lililoko nchini Ethiopia. Hata hivyo, wataalamu wanasema kwamba Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee linazolitofautisha na lile lililoko Ethiopia.
Moja ya tofauti hizo ni kwamba Ziwa Ngosi limezungukwa na milima na misitu minene tofauti na lile la Ethiopia ambalo liko eneo lililo wazi na hufikika kwa urahisi kabisa kwa gari kitu ambacho hakiwezekani kwa Ziwa Ngosi. Wataalamu wanasema kwamba kuwepo kwa ziwa hilo sehemu hiyo kunasaidia kuzuia milipuko ya mara kwa mara ya volkano kwa kuwa linasaidia kupunguza misukumo ya gesi inayojijenga chini na kuanza kutafuta upenyo wa kutokea chini ya ziwa.
Zipo imani nyingi potofu juu ya ziwa hilo la maajabu watu
husema ziwa hili lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli
kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya
mara kwa mara kitu ambacho si sahihi kitaalam ziwa haliwezi kuhama, Zipo
imani miongoni mwa watu kuwa ziwa Ngosi watu wanapotea kimazingara,
kuwapo kwa sauti za watu wasioonekana ndani ya misitu, wengine husema
ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za
kijani, bluu, nyeusi na nyeupe kitu ambacho kinawafanya waamini kuwa
ziwa hilo sio la kawaida.
Ni vyema ukatembelea ziwa hilo uoene maajabu na mvuto wa asilia wa Ziwa Hili
0 Maoni:
Post a Comment